Wamiliki
wa magari wametakiwa kutoruhusu magari
mabovu ya safari za mikoni kuingia mkoani katavi kutoa huduma ya usafiri.
Mkuu
wa polisi kikosi cha usalama
barabarani mkoa wa katavi willy Joas Mwamasika amesema hayo wakati
akizungumza na Mpanda Redio na kusema kuwa baadhi yao wamekuwa wakiufanya mkoa
wa katavi kama dampo la magari mabovu.
Amesema
watu wamekuwa wakikiuka sheria za usalama barabarani kutokana na mazoea
yaliyokuwepo tangu mwanzo hivyo kutokana na oparesheni ya nyakuanyakua itaondoa
mazoea hayo.
Hivi karibuni Kamanda wa Kikosi cha
Usalama Barabarani Tanzania, Fortunatus Musilimu, amesema dereva yeyote wa
mabasi yaendayo mikoani anayeshindwa kufuata sheria na alama za barabarani ni
vyema akaacha kufanya kazi hiyo kwa kuwa atakamatwa kwa mtindo wa ‘nyakua
nyakua’.
No comments:
Post a Comment