Ulinzi
wa polisi jamii na ulinzi shirikishi katika kata ya Majengo Manispaa ya Mpanda
Mkoani Katavi,Umeanza baada ya taratibu za kuunda vikundi
kukamilika.
Katika
Mahojiano na Mpanda Radio,Mkuu wa kituo cha polisi Wilaya ya Mpanda Milton
Sandari amesema tayari vikundi katika mitaa ya Majengo,Mji mwema na Maridadi
vimeandaliwa.
Kwa
upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Majengo John Salanda ameiambia Mpanda
Radio kuwa wao tayari wametekeleza agizo la Kamanda Nyanda la kuwataka kuandaa
Ofisi kwa ajili ya Polisi Kata ambapo amesema mpaka sasa hajaletwa.
Mei
25 mwaka huu,kamanda Nyanda kupitia mkutano wa hadhara katika kata ya Majengo,alimwagiza
Mkuu wa polisi kituo cha Polisi wilaya ya Mpanda Milton Sandari kuhakikisha
vikundi vya ulinzi shirikishi vinaundwa haraka ili kudhibiti uhalifu uliopo
katika kata hiyo.
No comments:
Post a Comment