Wafanyabiashara katika
soko kuu Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamesema utaratibu uliowekwa wa
kupata leseni ni changamoto katika kukamilisha masharti ya kufanya biashara.
Wakizungumza na Mpanda
Radio kwa nyakati tofauti wamesema wafanya biashara wengi wanashindwa kupata
leseni hizo kwa wakati kutokana na usumbufu wanaoupata katika mchakato wa
upatikanaji wa leseni hizo.
Hata hivyo wameiomba
serikali kuwapa muda wafanya biashara ili elimu ili kila mfanyabiashara aweze
kutambua umuhimu wa kulipia leseni hizo.
Hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Liliani
Charles Matinga alimpa wiki moja Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda kuhakikisha
kila mfanyabihashara anakuwa na leseni.
No comments:
Post a Comment