Jumuiya ya
wafanyabiashara mkoa wa Katavi imesema kuna mkwamo mkubwa wa kibiashara nchini
kutokana na kuongezeka kwa kodi na tozo
mbali mbali.
Hayo yameelezwa na
mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoani Katavi Aman Mahelah alipokuwa akizungumza na
Mpanda radio amesema suala la kutetea maslahi ya wafanya biashara limekwamishwa
na kukosekana kwa uelewa wa pamoja kati ya serikali na wafanyabishara.
Pamoja na hayo
amezitaja baadhi ya changamoto zinazo ikabili jumuia hiyo kushindwa kupata
majibu sahihi kutoka serikalini ambapo baadhi ya watendaji wa serikali hugeuzwa madai hayo kuwa ni ya wapinga maendeleo na wakwepa
kodi
No comments:
Post a Comment