Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Swalehe Mbwana Muhando amewataka wakulima wa zao
la Pamba wilayani humo kujiandaa na msimu wa mauzo .
Muhando ametoa Kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa
habari na kufafanua kuwa serikali
inaendelea na utaratibu wa awali ili kutangaza rasmi tarehe ya ununuzi.
Katika hatua nyingine amezionya baadhi ya kampuni zinazo
jihusisha na ununuzi wa zao hilo kuachana na vitendo vya udanganyifu kwenye
vipimo vinavyo tumika.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Mkoa wa Katavi kuuza pamba
tangu kuanzishwa kwa makakati wa kilimo cha mazao mbadala kama vile korosho,alizeti
na Pamba.
No comments:
Post a Comment