Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wametoa
maoni toafauti juu ya kuanzishwa kwa kampeni ya upimaji wa virusi vya ukimwi nyumba kwa nyumba.
Wakizungumza na Mpanda Radio wamesema kuwa kampeni
hiyo itasaidia katika kupunguza maambukizi mapya ya ugonjwa huo na kuongeza
uelewa wa wananchi waliokuwa na hofu ya kupima virusi vya ukimwi.
Aidha wametaja sababu za wanaume wengi kutokuwa
tayari kupima kuwa ni pamoja na uoga kutokana na wengi wao hujikuta katika
wimbi la ngono isiyo salama.
Kwa
mujibu wa Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema Serikali imeandaa kampeni maalum ya kuhamasisha upimaji wa
VVU na kuanza matumizi ya dawa za kufubaza VVU mara moja hususani
kwa wanaumena na SS Kampeni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa jijini Dodoma
tarehe 19 Juni mwaka huu.
CHANZO:Restuta Nyondo
No comments:
Post a Comment