Wazazi wametakiwa
kuacha tabia ya kuwashawishi watoto wao kufanya vibaya katika mitihani kwa
lengo la kuwaozesha ili wapate mahari.
Kauli hiyo ameitoa mkuu
wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando ambapo amesema wazazi wamekuwa
wakichangia kwa kiasi kikubwa kurudisha Maendeleo ya wanafunzi nyuma hususani
wanafunzi katika shule za msingi.
Mhando amesema kila
mmoja anawajibu wa kuhakikisha anashiriki katika kuinua elimu ili wanafunzi wafikie
ndoto zao hivyo hatua kali zitachukuliwa kwa wazazi ambao watabainika
kuwakatisha wanafunzi masomo.
Kwa mujibu wa Takwimu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, wasichana 8000 kila mwaka huacha shule kutokana na ujauzito na Kati yao 3,000 ni wanafunzi wa shule za
msingi.
CHANZO:Rebecca Kija
No comments:
Post a Comment