Wafugaji Mkoani
Katavi wameanzisha mpango wa kuwepo kwa chama
cha ushirika cha wafugaji kitakacho kuwa na uwezo wa kutatua changamoto za
wafugaji .
Wakizungumza katika
kikao cha mchakato huo katika ukumbi wa mikutano wa galden wamesema kuanzishwa
kwa ushirika huo kutawasaidia watambulike
kisheria
Mwenyekiti wa wafugaji mkoa wa Katavi Mussa Kabushi amesema umoja huo
utawaunganisha pamoja na
kurahisisha upatiakaji wa masoko kwa
mifugo .
Mkoa wa Katavi unatajwa kuwa na idadi kubwa ya wafugaji
sambamba na shughuli za kilimo kutokana na jiografia ya mkoa.
CHANZO:Paul Mathius
No comments:
Post a Comment