MPANDA
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya
Kasokola iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wanalazimika kusomea katika
vyumba vya maabala vyenye kemikali za kisayansi zinazotumika kwa ajili ya
masomo ya fikizikia,Kemia na baiolojia.
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo
ambao wamezungumza na Mpanda Radio,wameiomba serikali na wadau kujenga vyumba
vya madarasa ili kuwaepusha na mazingira hatarishi walimu na wanafunzi.
Kwa upande wake Kaimu mkuu wa shule
ya sekondari Kasokola Joel Mwandwanda amesema wanafunzi kusomea katika vyumba
vya maabala kunatokana na uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo.
Kwa mjibu wa kaimu Mkuu wa shule hiyo
yenye wanafunzi 415 iliyoanzishwa tangu mwaka 2008 ina upungufu wa walimu hasa katika
masomo ya Sayansi ambapo kwa sasa kuna walimu wawili mmoja akifundisha
hisababti na mwingine Kemia kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne.
Chanzo:Isack Gerald
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment