KATAVI
Wananchi mkoani Katavi
wamevipongeza vyombo vya habari
kwa kuhabarisha umma kuhusu mambo mbali mbali ya kimaendeleo katika jamii.
Wameeleza kuwa kupitia redio wananchi wamepata upeo wa kujua nguvu ya kusema na kukosoa inavyo chochea Uwazi na uwajibikaji miongoni mwa jamii na serikali.
Halikadharika
wameshauri vyombo vya habari nchini
kujikita na vipindi vinavyoelimisha na vinavyojenga maadili kwani vyombo
vya habari ndiyo kioo cha jamii na taifa kwa ujumla.
Maadhimisho ya redio kitaifa yamefanyika
mjini Dodoma na kujumuisha waandishi wa vyombo
vya habari vya jamii kutoka Tanzania bara na visiwani.
Kauli mbiu ni usawa wa kijinsia katika michezo na kutangaza michezo pamoja na kuhusisha amani kupitia michezo.
Chanzo:Adelina Ernest
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment