MPANDA
Wakazi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameitaka serikali kuendelea kutoa elimu juu ya
maswala ya unyanyasaji wa kijinsia ili kupunguza vitendo hivyo.
Miongoni mwa wananchi waliozungumza na Mpanda Redio wameeleza kuwa chanzo
cha ukatili wa kijinsia ni kutokana na kushamiri kwa mfumo dume mkoani hapa.
Emannuel Thobias Lindege mkuu wa dwati la jinsia na watoto kituo cha
polisi Mpanda amesema wananchi wamekuwa wakipata elimu juu ya kupinga ukatili huo kupitia kwa
wahanga waliokumbwa na matukio kama hayo.
Mkoa wa katavi miongoni mwa mikoa inayotajwa kuwa kinara wa matukio ya
unyanyasaji wa kijinsia kama vile mimba za utotoni.
Chanzo: Furaha Kimondo
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment