NSIMBO
Zaidi ya wanafunzi 160 wa
shule ya sekondari machimboni iliyopo kata katisunga halmashauri ya Nsimbo
mkoani Katavi wanalazimika kulala katika jengo dogo la hostel lililopo shuleni
hapo.
Mpanda radio imezungumza na baadhi ya wanafunzi hao na kusema kuwa wanalazimika kulala wawili hadi watatu katika kitanda kimoja na wengine kulala chini.
Kwa mujibu wa mlezi wa
wanafunzi wa kike wa shule hiyo Mwalimu
Restuta Msafiri amesema jengo la hostel hiyo lina uwezo wa kulaza wanafunzi 48
tu lakini kutokana na mahitaji wanalazimika kulaza zaidi ya wanafunzi 160
Katika hatua nyingine
Mwalimu Msafiri ameiomba serikali kusaidia ujenzi wa mabweni ili kupunguza
utoro na mimba kwa wasichana
Pamoja na kuwa na jengo
moja la hosteli ya wasichana ambalo pia halitoshelezi shule ya sekondari
Machimboni ina zaidi ya wanafunzi 600 wanaotoka katika vijiji vya Katsunga,
Ibindi na Itenka
Chanzo:Paul Mathias
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment