Mwandishi Wetu Furaha Kimondo aikwa na mnuaika na Tasaf kata ya kibaoni |
MPIMBWE.
Serikali
ya kijiji cha Ilalanguru iliyopo kata ya Kibaoni Halmashauri ya Wilaya ya
Mpimbwe imetakiwa kuwashauri walengwa kutumia fedha wanazopata kama mpango
unavyotaka ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Ameyasema
hayo mratibu wa tasaf Lucas Kombe wakati
akizungumza na mpanda radio na kusema kuwa mpango wa kunusuru kaya maskini una
lengo la kuzitoa kaya hizo katika hali ya chini na kuzifikisha kwenye mafanikio
lakini walengwa wengi wamekuwa wakizitumia kinyume na mpango unavyotaka.
Kwa
upande wa watendaji hao wamekubaliana na mratibu huyo na kuahidi kuanza zoezi
hilo mwezi ujao wakati wa kugawa fedha hizo.
Mpango
wa kunusuru kaya maskini ulianza tangu
mwaka 2014 mpaka sasa na katika Wilaya ya Mpimbwe kaya zinazonufaika na mpango
huo ni 2285 ambazo mafanikio yake ni sawa na asilimia 90% tangu kuanzishwa kwa
mradi huo.
Chanzo:Furaha
Kimondo
No comments:
Post a Comment