Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga |
KATAVI
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga ametoa wito kwa wakazi
waishio katika maeneo yasiyo rasmi wilayani Tanganyika kujenga katika maeneo
yaliyorasimishwa ili kupatiwa kuhuduma za kijamii.
Muhuga
ameto wito huo mwishoni mwa wiki wakati wa kikao cha wadau wa elimu wilayani
Tanganyika kikao ambacho kilifanyika Mpanda Mjini.
Ametaja
baadhi ya wakazi wanaotakiwa kujenga maeneo yaliyorasimishwa kuwa ni pamoja na
waliopo eneo la uwekezaji la Luhafwe kunakojengwa mji wa kisasa wa kibiashara.
Kwa
upande wake Mkuu aw Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando amesema kwa sasa inakuwa
vigumu kuwahudumia wakazi waliopo katika maeneo yasiyo halali kwa kuwa hata
hivyo wametawanyika sana.
Fedha
na vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya sh.millioni 152 zilizochangwa na wadau
hao kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto mbalimbali za kielimu wilayani
Tanganyika.
No comments:
Post a Comment