MPANDA
Baadhi ya wananchi halmashauri ya
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wamesema kuwa alama za usalama barabarani
ambazo zimewekwa katika barabara za ndani ya Manispaa zimepunguza ajali
ukilinganisha na siku zilizopita.
Wakizungumza na Mpanda Radio,Pamoja na
mambo mengine wameshauri elimu ya matumizi sahihi ya alama hizo iendelee
kutolewa kwa wananchi wote wakiwemo waendesha vyombo vya moto na watembea kwa
miguu.
Kwa mjibu wa wakazi wa Manispaa ya
Mpanda,mwaka uliopita maeneo yaliyokuwa hatarishi kwa wananchi ni pamoja na
maeneo ya shule,eneo la Super City kata ya Majengo na sokoni ambapo kulikuwa kukitokea ajali za mara kwa
mara kutokana na kutokuwepo kwa alama muhimu za barabarani.
Hata hivyo jeshi la Polisi kitengo cha
usalama barabarani mkoani Katavi,limekuwa likitoa elimu kupitia mikutano ya
hadhara na vyombo vya habari ikiwemo Mpanda Radio Fm kwa ajili ya kutambua
namna ya kuzuia ajali zisizo za lazima.
Chanzo:Issack Gerald
No comments:
Post a Comment