MPANDA
Wananchi wa kata ya kawajense
halmashauri ya manispaa mpanda mkoani katavi wameiomba serikali kutoa elimu juu
ya vitambulisho vya uraia.
Wameyasema hayo wakati wakizungumza na
mpanda radio na kusema kuwa hawana uelewa wa kutosha kuhusu utambulisho wa
uraia na kuomba kupewa elimu hiyo kabla ya kuanza kwa mchakato wa uandikishwaji
mkoani hapa.
Mfumo wa Kitambulisho cha Taifa bado ni dhana ngeni
miongoni mwa watu wengi hususani umuhimu wake kwa mwananchi, Taasisi mbalimbali
na Serikali kwa ujumla hali inayopelekea baadhi kudhani kuwa kitambulisho cha Uraia ni Kitambulisho kama
vilivyo vitambulisho vingine vya kazi.
March 6 mwaka huu
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Lilian Matinga amewaapisha wasimamizi wa zoezi la uandikishwaji wa
vitambulisho vya taifa mkoani Katavi.
Source:Restuta Nyondo
No comments:
Post a Comment