MPANDA
Wanachama wa kikundi cha Trans
Cargo wamewalalamikia wafanyabiashara kwa kuwalipa fedha kidogo kwa malipo ya
ubebaji wa mizigo ikiwa ni tofauti na bei elekezi ya serikali wanayotakiwa
kulipwa.
Wameyasema hayo wakati
wakizungumza na mpanda radio na kusema
kuwa kuwepo kwa bei hizo imekuwa ni changamoto kwao katika kuendesha maisha
yao.
Kwa upande wake mmoja wa
wafanyabiashara hao amesema kuwa malipo ya wabebaji hao ni maelewano baina ya
mbebaji na mfanyabiashara.
Hata hivyo mwenyekiti wa kikundi
hicho ameiomba serikali kuwasaidia kutatua changamoto hiyo ili kukifanya
kikundi hicho kikue zaidi.
Trans cargo ni kikundi cha wabeba
mizigo ambacho kina wanachama 70 na lengo lake ni kuwasaidia vijana kupata
ajira ili kujiokomboa na wimbi la umaskini na kinatambulika kisheria kwa kupewa
leseni ya biashara ambayo inawafanya kulipa kodi ili kuliongezea pato taifa.
Chanzo:Furaha Kimondo
No comments:
Post a Comment