NSIMBO
Baadhi ya wachimbaji wadogowadogo katika kata ya ibindi halmashauri ya simbo
mkoani katavi wameeleza
kutoridhishwa na mislahi
yatokanaya na uchimbaji wa madini.
Wamebainisha hayo wakati wakizungumza na
mpanda redio na kusema kuwa mfumo wa upangaji wa bei ya madini si rafiki kwao
kwani wakati mwinhine hutokea udanganyifu kuhusu bei hiyo.
Aidha wamekiri kuwepo kwa mabadiliko
katika sekta ya madini tofauti na awamu nyingine za uongozi kutokana na
kutofukuzwa ovyo kwenye machimbo wayovumbua madini.
Hivi karibuni rais wa tanzania john
magufuli amesaini sheria mpya ya madini itakayo wezesha serikali kumiliki
angalau asilimia 16 ya miradi ya uchimbaji wa madini na kuongeza kodi ya
mirahaba, akiapa kwamba sasa nchi yake haitaibiwa tena.
Chanzo:Ester Baraka
No comments:
Post a Comment