RUKWA
Mwanakwaya wa kwaya ya Mtakatifu Secilia,
Kigango cha Muze Parokia ya Zimba, Jimbo Katoliki Sumbawanga, Flora Nandi (25)
ameanguka na kufariki dunia muda mfupi baada ya kutoa sadaka ya shukrani akiwa
kanisani.
Tukio hilo limetokea siku
ya Jumapili saa nne za asubuhi wakati wa ibada ya kwanza
, kwaya ya Mtakatifu Secilia ikimsifu
Mungu katika ibada hiyo.
Akizungumzia tukio hilo,
mwalimu wa kanisa aliyekuwa akiongoza ibada hiyo, Katekista Philipo Lupadasi
amesema wanakwaya wakiwa wanaimba na marehemu akiwa ametoka kutoa sadaka ya
shukrani na kuendelea kuimba ghafla alianguka chini hali iliyozua mshtuko na
kusababisha ibada kusimama kwa muda.
Amesema baada ya kufikishwa
katika zahanati hiyo alipokewa na wahudumu wa afya ambao baada ya kumfanyia
uchunguzi walibaini kuwa alikuwa ameshafariki dunia.
Chanzo:Mwananchi
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment