Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni RPC, Muliro Jumanne Muliro |
DAR ES SALAM
Kamanda wa polisi mkoa wa
kipolisi Kinondoni RPC, Muliro Jumanne Muliro awaonya na kuwataka wasiasa
kufanya kampeni zao kistaarabu bila kuvunja sheria za nchi.
Kamanda Muliro amesema wamejipanga kuhakikisha uchaguzi wa Jimbo la
Kinondoni hauna nafasi yakuvunja amani na sheria za nchi kwakua taratibu na
kanuni zilizowekwa na serikali zinafuatwa na hawatasita kumchukulia hatua za
kisheria mtu yeyote atakayeonekana kukiuka sheria za nchi.
Kamanda Muliro amesema
wanatambua umuhimu wa zoezi hilo hivyo watagawa askari kulingana na ukubwa wa
eneo na wingi wa wapiga kura.
Chanzo:Eatv
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment