Monday, 14 May 2018

KAKOSO ATOA NENO BAADA YA KUPEWA GARI NA WIZARA


Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Selemani Kakoso ameishukuru serikali kwa kumpatia gari ambalo litamrahisishia  kukamilisha shughuli zake za kiutendaji jimboni kwake.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Mpanda Radio     na kusema kuwa gari hilo litawasaidia watendaji wake katika shughuli za doria hasa katika maeneo ya hifadhi ili kuzuia wawindaji haramu.

Aidha Kakoso amewataka wananchi kutunza chakula kilichopo na vyanzo vya maji kwa ajili ya kuwasaidia katika ukuaji wa maendeleo katika wilaya ya Tanganyika na hasa katika maeneo ya hifadhi.

Utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji vinasaidia kuwepo kwa uoto wa asili na pia huleta mvua na ni jukumu lakila mtu kutunza mazingira hayo.

CHANZO:Alinanuswe Edward

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...