Chama cha wakulima wa
Tumbaku cha Mpanda Kati katika
halmashauri ya wilaya ya Mpanda kimetoa mifuko hamsini ya saruji yenye thamani
ya shilingi million moja kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za
maendeleo.
Kiasi hicho cha saruji
kimekabidhiwa kwa halmashauri hiyo na Bw.Mashaka Shanani kwa niaba ya bodi ya
chama kama kutimiza ahadi waliyoitoa wakati wa kikao cha wadau wa elimu
kilichofanyika Machi 10 mwaka huu mjini Mpanda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Rojas
Lumury,amekishukuru chama hicho kwa msaada huo ambao utasaidia kutatua
changamoto kadhaa za masuala ya kielimu katika halmashauri hiyo.
Katika kikao hicho cha
wadau wa elimu,zaidi ya shilingi milioni 152 zilipatikana baada ya kuchangwa na
wadau mbalimbali wa maendeleo kwa ajili ya kutatua changamoto za miundombinu ya
shule za Wilaya ya Tanganyika
CHANZO:Paul
Mathias
No comments:
Post a Comment