Tatizo la uelewa kwa
watoto wa kike hususani ambao wapo katika ngazi ya elimu ya msingi juu ya namna
ya kujistiri pindi wanapokuwa wamefikia umri wa kupevuka imekuwa changamoto
kubwa na kusababisha kushindwa kuhudhuria masomo.
Mwalimu wa Shule ya
Msingi Mpanda Yusta Sanga iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi amesema watoto wa kike wamekuwa
wakishindwa kuhudhuria masomo kutokana na kupata maumivu makali au kukosa vifaa
vya kujistiri kama vile taulo.
Aidha ameiomba Serikali
isaidie kutoa vifaa vya huduma ya kwanza kwani
vilivyopo havitoshelezi hasa kwa
shule za msingi.
Watoto wengi wa kike wamekuwa wakikosa vipindi shuleni
pindi wanapokuwa katika siku za hedhi kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo
ukosefu wa taulo na kupata maumivu makali ya tumbo.
CHANZO:Johari Secky
No comments:
Post a Comment