Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA)
imetoa tahadhari ya kunyesha mvua kubwa kwa siku tano kuanzia jana, ambazo
zinaweza kuleta mafuriko katika maeneo ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani,
Lindi, Mtwara na Visiwa vya Unguja na Pemba.
Katika
taarifa ya TMA iliyotolewa Mei 13, mvua hizo zilizoanza kunyesha
zitaendelea mpaka Mei 17 mwaka huu.
TMA
imesema athari zinazinaweza kutokea ikiwemo mafuriko ambayo yanaweza kusababisha
kuvurugika kwa usafiri, barabara kubwa kutopitika na maisha ya watu kuwa
hatarini kutokana na maji kujaa au kupita kwa kasi.
Aidha
imetoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea
kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zitakazotolewa.
No comments:
Post a Comment