Tuesday, 6 February 2018

Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imesema haitasita kuvifungia vituo vya elimu vinavyotoa mafunzo kabla ya kusajiliwa.



 

MPANDA

Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imesema haitasita kuvifungia vituo vya elimu vinavyotoa mafunzo kabla ya kusajiliwa.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Elimu Taaluma wa Manispaa ya  Mpanda Mwalimu Rashid Pili,wakati akizungumza na Mpanda Radio kuhusu mwafaka wa kikao baina ya serikali na wamiliki wa vituo hivyo vinavyotoa huduma ya elimu kwa wanafunzi bila usajili wa serikali.

Wiki iliyopita Halmashauri iliwatahadharisha wazazi kutopeleka watoto wao katika vituo ambavyo havijasajiliwa kwa kuwa wanafunzi watakuwa hawatambuliki katika mfumo wa elimu Tanzania na hivyo kupoteza haki yao.

Kwa mjibu wa Afisa elimu,kuna vituo vipatavyo 15 vinavyotoa elimu bila kusajiliwa ambapo leo Februari 5 ndiyo ilikuwa mwisho wa vituo hivyo kutimiza masharti waliyoafikiana ikiwemo kuvisajili.

Chanzo:Rebecca Kija
#Changia Damu Okoa Taifa

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...