Tuesday, 6 February 2018

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amemtaka kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Arnord Msuya kumsimamisha kazi Ofisa Tarafa ya Dongobesh, Bayo Banka



 

Mkuu wa Mkoa wa Manyara  Alexander Mnyeti

 

MANYARA

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amemtaka kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Arnord Msuya kumsimamisha kazi Ofisa Tarafa ya Dongobesh, Bayo Banka kwa madai ya kushindwa.

Pia, amewataka watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ambao hawaungi mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kuacha kazi vinginevyo atawachukulia hatua kwa kutotimiza wajibu wao ipasavyo na kuingiza siasa kazini.

Amesema Banka anapaswa kusimamishwa kazi hadi hapo atakapotoa maelezo ya kushindwa kutimiza wajibu wake kwa kuchanganya siasa na kazi. 

Mnyeti amesema anayo majina na taarifa za baadhi ya watumishi wanaofanya kazi kizembe na kuzorotesha  shughuli za Serikali.

Chanzo:Mwananchi

#Changia Damu Okoa Taifa

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...