Tuesday, 6 February 2018

Baadhi ya wanasheria na wanaharakati wameeleza kufurahishwa na uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ya kumwondolea Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) mamlaka ya kuzuia dhamana ya mshtakiwa bila hata kulazimika kutoa sababu



 

DAR ES SALAAM.

 Baadhi ya wanasheria na wanaharakati wameeleza kufurahishwa na uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ya kumwondolea Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) mamlaka ya kuzuia dhamana ya mshtakiwa bila hata kulazimika kutoa sababu.

Mahakama hiyo imebatilisha kifungu cha 148 (4) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, kinachompa mamlaka hayo DPP kupitia hukumu ya rufaa ya Mwanasheria Mkuu dhidi ya mwanaharakati wa haki za binadamu, Jeremiah Mtobesya.

Baadhi ya wanasheria wamesema hatua hiyo itasaidia kulinda haki za watuhumiwa wanaohukumiwa kabla ya kupatikana na hatia.

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo Bisimba amesema mamlaka ya DPP yalikuwa yakitumika vibaya kukandamiza haki za watuhumiwa.

 Chanzo:Mwananchi

#Changia Damu Okoa Taifa

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...