Tuesday, 6 February 2018

Mkuu wa KKKT awataka washarika Mtwara kuwa watulivu


Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Fredrick Shoo  
Moshi. 
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Fredrick Shoo amewataka washarika wa Kanisa Kuu la Mtwara kuwa na subira wakati akijiandaa kwenda kuzungumza nao.
Dk Shoo, ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini alisema jana kuwa amepanga kwenda kuwaona kama walivyoomba, lakini akawataka wadumishe upendo na kumtumikia Mungu kama Wakristo wamoja.
Alisema hayo jana alipozungumza na Mwananchi ikiwa ni siku moja baada ya Askofu wa Dayosisi ya Kusini Mashariki, Dk Lucas Mbedule kuwaomba msamaha washarika wa kanisa hilo la Mtwara.
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wamekuwa wakimpinga askofu huyo kwa takriban miaka miwili lakini juzi Dk Mbedule aliwaangukia na kuwaomba msamaha wote aliowakosea ili wasiliumize kanisa.
“Nimewakosea mengi siwezi kuhesabu kabisa. Mimi ni mwenye dhambi kabisa kabisa sistahili kabisa. Naomba mnisamehe tusilitese kanisa. Kama kuna jambo njoo tuzungumze,” alisema Dk Mbedule.
Akiwa katika ibada juzi, askofu huyo alisema watakapoweka vizuri utaratibu, Dk Shoo atakwenda kuwasalimia na kuzungumza nao kwa kuwa mazungumzo yanaruhusiwa ila yasiharibu utaratibu.
Kabla ya kutoa kauli hiyo, msaidizi wa askofu, Mchungaji Yeriko Ngwema alimuita mmoja wa waumini, Steven Macha ambaye alimtaka askofu kuitisha majadiliano ili kumaliza mgogoro huo.
Chanzo:Mwananchi
#Chngia Damu Okoa Taifa

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...