Tuesday, 6 February 2018

Chama cha mapinduzi ccm katika Halmashauri wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi kimeazimisha miaka 41 ya kuasisisiwa kwa chama hicho kwa kutembelea Gereza la kilimo la Kalila nkulunkulu na kutoa msaada wa mahitaji kwa wafungwa.



TANGANYIKA

Chama cha mapinduzi ccm katika Halmashauri wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi kimeazimisha miaka 41 ya kuasisisiwa kwa chama hicho kwa kutembelea Gereza la kilimo la Kalila nkulunkulu na kutoa msaada wa mahitaji kwa wafungwa.

Katika ziara hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Tanganyika Yasini Mohamedi Kibiliti amesema wameguswa na changamoto wanazo zipata wafungwa za kutokuwa na mahitaji madogo madogo ya kujikimu katika maisha yao ya kila siku ndomaana wamewatembelea na kutoa mahitaji mbalimbali kama sukari na sabuni

Askari wa geleza hilo Asp James Sapi ameshukuru kwa niaba ya Mkuu wa geleza hilo kwa  chama hicho kutambua umuhimu wa kuwatembelea wafungwa na kutoa msaada ambao utawasaidia kujikimu katika mahitaji na kuziomba taassi zingine kujitokeza katika kujitolea mahitaji kwa wafungwa hao.

Chama cha Mapinduzi ccm kiliasisiwa rasimi 5/2/1977 baada ya muungano wa vyama viwili vya Asp upande wa zanzibari na TANU upande wa Tanzania bara na kuzaliwa chama cha mapinduzi ccm. 

Chanzo:Paul Martius 

#Changia Damu Okoa Taifa

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...