Monday, 2 April 2018

TANESCO KATAVI YAFAFANUA MFUMO MPYA WA UNUNUZI UMEME


KATAVI


Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoani Katavi  limesema Mfumo mpya wa unuaji umeme kupitia GePG wenye lengo la kuwepo kwa uwazi juu ya uendeshaji wa taasisi za serikali pamoja na matumizi hautamuathiri Mteja

Meneja Uhusiano wa wateja mkoani Hapa Amoni Maiko  Amebainisha hayo wakati akizungumza na Mpanda radio  na kuongeza kuwa GePG atakuwa wakala wa katikati baina ya Tanesco na muuzaji wa umeme na atakayetaka kuuza umeme ni lazima kwenda GePG ndipo aunganishwe na Tanesco.

Amesema kupitia mfumo huo mtu yeyote anayetaka kuuza umeme lazima auze kupitia GePG na hautokuwa na athari kwa wateja wake kwani umeongeza idadi ya wauzaji tofauti na ilivyokuwa awali.

 CHANZO:Edward Mganga 


No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...