Mchungaji Shakiland Foya wa Kanisa La KKKT usharika wa Mpanda Mjini Akihubiri katika ibada ya Pasaka
Viongozi waliopewa nafasi ya kuongoza
katika Taifa kupitia Nyanja mbalimbali wametakiwa kusimamia nafasi zao katika kutenda haki
Akizungumza baada ya ibada ya Pasaka Mchungaji wa
Kanisa wa KKKT Usharika wa Mpanda mjini Mchungaji
Shakiland Foya amewasihi Viongozi hao huku akibainisha kuwa haki huinua Taifa.
Aidha amewataka watanzania kupendana
na kudumisha amani, huku wakiamini kuwa kifo na hatimaye kufufuka kwa Yesu
Kristo, ni ishara tosha kwamba mwisho wa matatizo yanayomkabili kila mtu katika
maisha yake umekaribia.
Akifafanua salamu zake hizo
mchungaji Foya amesema kama ilivyotokea
kwa Yesu Kristo, watanzania na hususani waumini wa dini ya Kikristo wanapaswa
kuwa na imani kuwa matatizo pamoja na shida mbali mbali zinazowakabili mwisho
wake umekaribia.
CHANZO:Edward Mganga
No comments:
Post a Comment