![]() |
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Dkt. Vincent Mashinji |
Thursday, 4 January 2018
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Vincent Mashinji amesema kuendelea kuhama kwa Madiwani na baadhi ya wanachama wa chama hicho chanzo chake ni rushwa na sio sababu nyingine kama wao wanavyotoa.
DAR
ES SALAAM
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo, (CHADEMA) Dkt. Vincent Mashinji amesema kuendelea kuhama kwa Madiwani
na baadhi ya wanachama wa chama hicho chanzo chake ni rushwa na sio sababu
nyingine kama wao wanavyotoa.
Kauli
hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Vincent Mashinji leo
kufuatia kujiuzulu kwa madiwani wawili
wa CHADEMA Mkoani Iringa na kujiunga na Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Aidha
katibu huyo wa CHADEMA ameendelea kwa kusema sio tu madiwani ambao wanafatwa na
kupewa rushwa bali hata kuna wabunge na viongozi wa juu kabisa ambao wanafatwa
na kushawishiwa kwa kupewa rushwa.
Mpaka
sasa Manispaa ya Iringa Mjini imepoteza madiwani wa Kata sita ambao wote baada
ya kujiuzulu wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Source Mwananchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Featured post
MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO
Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio ...
-
Kabale, Uganda. Mpinzani mkuu wa Uganda na kiongozi wa Forum for Democratic Change (FDC) Dk Kizza Besigye amekamatwa. ...
-
Serikali ya mtaa wa Kampuni Kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imewaomba wataalamu wa maji Manispaa ya Mpanda kuchungu...
-
NSIMBO Soko la Katumba Mnyaki linalomilikiwa na halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi halina choo tangu kuanzishwa kwake hali...

No comments:
Post a Comment