Thursday, 4 January 2018

Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu amekiri kutofanyika kwa maadhimisho ya siku ya walemavu duniani kwa mwaka uliopita kutokana na kutokuwa na mawasiliano ya kutosha kati ya halmashauri hiyo na ofisi ya mkoa.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu

MPANDA

Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu amekiri kutofanyika kwa maadhimisho ya siku ya walemavu duniani kwa mwaka uliopita kutokana na kutokuwa na mawasiliano ya kutosha kati ya halmashauri hiyo na ofisi ya mkoa.

Alizungumza na Mpanda Redio kwa njia ya simu Bwana Nzyungu alesema mkoa ndio wenye jukumu la kupanga sherehe  katika ngazi ya halmashauri na wilaya jambo ambalo halikufanyika.

Katika hatua nyingine  amesema kuwa suala la bajeti  sio tatizo kiasi cha kukwamisha maadhimisho hayo na kuahidi kuwa mwaka huu manispaa itahakikisha tatizo hilo halijirudii tena.
Mkoa wa katavi umeshindwa kuaandaa Maadhimisho ya siku ya walemavu duniani miaka miwili mfululizo ambayo hufanyika desemba tatu kila mwaka.
Chanzo: Ester Baraka

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...