KATAVI
Chama cha
Walimu Tanzania(CWT) mkoa wa Katavi kimempongeza
rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwa kutangaza kutoa fedha bilioni 200
ili zilipe madeni ya ndani yakiwemo ya walimu.
Akizungumza
na Mpanda radio fm kwa njia ya simu katibu wa chama cha CWT mkoa wa Katavi
mwalimu Hamiss Chinahova amesema hatua ya serikali kulipa madeni hayo italeta
mageuzi makubwa katika sekta ya elimu.
Katika hatua
nyingine amewataka waalimu kuendelea kujituma na kufanya kazi kwa weledi zaidi
ili ilete tija kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Mwaka 2017
walimu nchini Tanzania walitishia kugoma kwa kile walicho kitaja kuwa ni
kukithiri kwa madai dhidi ya serikali wakisema inawavunja morari ya kazi.
Chanzo: Alinanuswe Edward
No comments:
Post a Comment