Saturday, 31 March 2018

“ENDELEZENI MEMA YOTE KAMA MLIVYOKUWA MKIFANYA KIPINDI CHA KWARESMA"-ASKOFU


KATAVI
Mhashamu Baba Askofu Gervas Nyaisonga, wa Jimbo Katoliki la Mpanda Mkoani Katavi

Mhashamu Baba Askofu Gervas Nyaisonga, wa Jimbo Katoliki la Mpanda Mkoani Katavi  amewataka waumini wa kikristo kuendelea  kutenda mema kama walivyofanya katika kipindi cha mfungo wa Kwaresma.
Askofu Nyaisonga ametoa wito huo katika maadhimisho misa takatifu ya Ijumaa kuu ibada ambayo imefanyika katika Kanisa kuu la Bikira Maria Emakulata Jimbo la Mpanda.
Kwa upande wao waumini wa kanisa hilo wamesema kipindi cha Kwaresma ni kipindi cha kutafakari wema ambao Mungu ameuonesha kwao na hivyo kutakiwa kutenda hivyo hivyo kwa wenye uhitaji.
Ijumaa Kuu  ambayo kitaifa imeadhimishwa mkoani Mbeya ni siku maalumu ya mwaka ambayo wafuasi wengi wa Yesu Kristo wanaadhimisha kifo chake msalabani ambacho kilitokea nje ya kuta za mji wa Yerusalemu siku ya Ijumaa ambapo inatanguliwa na Alhamisi Kuu.
Sikukuu ya pasaka Jumapili ya Aprili mosi mwaka huu,Watanzania wataungana na wakristo wengine duniani kote katika maadhimisho siku hiyo muhimu katika ukristo.
Chanzo: Restuta Nyondo

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...