MPANDA
Matukio ya ukatili wa kinjisia
yamepungua kwa asilimia kubwa katika
manispaa ya Mpanda Mkoni Katavi tofauti na kipindi cha mwaka jana.
Hayo yamesemwa na Coplo Judith Mbukwa kutoka katika dawati la jinsia
mkoani katavi wakati akizungumza na mpanda radio kwa njia ya simu ambapo amesema kesi za ukatili wa kinjisia zimepungua kutokana na
wanaoriport kuwa wachache.
Pia amesema kuwa dawati la jinsia
limeanza kutoa elimu kwa wananchi mkoani kote kwa lengo la
kuelimishana,kushirikiana na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika
semina zinazotolewa na dawati hilo ili wapate elimu husika juduithi ametoa wito
kwa wananchi kutoa taarifa pindi maswala ya ukatili yanapotokea katika
mazingira yao .
Ukatili wa kijinsia ni kitendo
anachofanyiwa mtu yeyote mwanamke au mwanaume kwa lengo la kumdhuru au
kumuumiza kisaikolojia,.
Hata hivyo tafiti nyingi zimeonyesha kwamba wanawake
na watoto ndiyo wahanga wakuu wa ukatili wa kijinsia
CHANZO:Ezelina Yuda
No comments:
Post a Comment