MPANDA
Vijana wa Chama cha Mapinduzi ccm
wilayani Mpanda wameonywa kutoingiza masuala ya udini na ukabila kwenye siasa.
Hayo yamesemwa na katibu wa umoja wa
vijana wa chama cha cha mapinduzi UVCCM Bwana Deus Thomas katika mkutano na
wananchi wa kata ya Kanoge
Bwana Thomas amewataka vijana
kujikita katika kutekeleza sera za chama hicho kwani ndizo zinazowaunganisha
Aidha ameongeza kuwa chama hakitasita
kuwachukulia hatua kali zikiwemo kuwafuta uanachama wale wote watakaobainika
kwenda kinyume na matakwa ya chama
CHANZO:RESTUTA
NYONDO
No comments:
Post a Comment