Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Kasimba
katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametaka vikundi vya
polisi jamii na ulinzi shirikishi mtaani hapo kufuata maelekezo waliyopewa ili
kudhibiti uharifu kuliko kupiga wananchi na kukamata pikipiki barabarani.
Malalamiko hayo yametolewa na wakazi
hao kwa nyakati tofauti wakati wakizungumza na Mpanda Radio ambapo pia wengine
wamesema uwepo wa vichaka vingi mtaani hapo kumechangia kuongezeka kwa uharifu.
Bw.Said Rashid Mdemela na Rejius Damiano Mwanisawa ni
miongoni mwa wananchi ambao wamezungumzia changamoto hiyo ya ulinzi.
Mwenyekiti wa mtaa wa Kasimba
Bw.Laurent Machimu amekiri polisi jamii kukikuka taratibu za ulinzi ambapo
amesema wamewaita na kuwaelekeza vizuri huku akisema viwanja vilivyopimwa na
kutelekezwa vimechangia kuficha waharifu.
Mtaa wa Kasimba wenye watu wapatao
2000 ni miongoni mwa mitaa mitatu ya kata ya Ilembo na mtaa huo una vikundi
viwili vya polisi jamii vyenye jumla ya vijana 43.
CHANZO:Ezalina Yuda
No comments:
Post a Comment