KATAVI
Jamii imetakiwa kuwa na ushirikiano
katika malezi hususani ngazi ya familia ili kumjengea mtoto mazingira rafiki ya
kitaaluma na nidhamu katika maisha.
Mwalimu Philbert Nguvumali ni Afisa
taaluma katika halmashauri ya wilaya ya mpanda mkoani katavi amesema kuwa
watoto wengi wamekuwa wakiathirika kisaikolojia kutokana na tatizo la kutengana
kwa wazazi au mtoto kupata malezi ya mzazi mmoja.
Nguvumali amesema kuwa watoto
wanaopata malezi ya mzazi mmoja hujikuta wakishindwa kuwa na uwezo mkubwa
wakufikiri na ni chanzo cha kuwa na tabia ya ubinafsi.
Imeelezwa kuwa katika nchi ya
Tanzania na kenya kati ya familia 10
kuna familia 7 za mzazi mmoja hususani
familia zinazoongozwa na mama pekee.
Chanzo :Restuta Nyondo
No comments:
Post a Comment