TANGANYIKA
Baadhi ya Wakazi wa kitongoji cha Kagwila kata ya Kabungu wamesema
bado kuna uhitaji mkubwa wa serikali kuendelea kutoa elimu ya ujenzi wa vyoo
bora ili kujikinga na magonjwa ya mripuko.
Hayo yamesemwa na baadhi ya wananchi katika kitongoji cha Kagwira kijiji cha kabungu wilaya Tanganyika Mkoani Katavi ambapo wamesema hawana elimu yoyote kuhusu umuhimu wa ujenzi vya vyoo bora katika makazi.
Faustina Maganga ambaye ni katibu wa kitongoji hicho ambaye amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kutaka serikali iendelee kuhamasisha jamii.
Mwaka 2017 Serikali iliutangazia umma kuhakikisha kila kaya inakuwa na
choo bora hii ni kufuatia zaidi ya mikoa 20 ya Tanzania kukumbwa na ugonjwa wa
kipindu pindu mwishoni mwa 2016.
Chanzo:Rebeca Kija
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment