MPANDA
Baadhi ya wanawake mkoani
katavi wamesema wanashindwa kutumia njia za uzazi wa mpango kutokana na kukosa
elimu sahihi juu ya uzazi.
Wanawake hao wameiambia mpanda Radio kuwa moja ya changamoto ni imani potofu na baadhi ya wanaume kutotaka kushiriki katika njia za uzazi wa mpango.
Kwa upande wake muuguzi anayesimamia huduma ya baba,mama na mtoto katika zahanati ya kata ya Kakese Yusuph Jabil Ally amesema kuwa wanawake wengi wamekuwa wanaogopa kupata ushauri juu ya ya njia salama za uzazi wa mpango
Bwana Ally ametoa wito kwa
wakazi kuachana na imani potofu juu njia za uzazi wa mpango ili kujikinga na
mimba zisizotarajiwa na kupanga familia ya watoto ambao watakuwa na uwezo wa
kuwatunza.
Chanzo: Restuta Nyondo
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment