Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ametaka hukumu ya kifo kurejeshwa nchini humo.
Matamshi yake yanakuja baada ya afisa wa wizara ya sheria, kufichua mwezi uliopita kuwa zaidi ya watu 50 washahukumiwa kifo.
Hukumu ya kifo ilitekelezwa mwisho nchini Zimbabwe mwaka 2005, wakati mtu ambaye alikuwa akiitekeleza kustaafu kwa mujibu wa shirika la AFP.
Akiongea wakati wa maziko ya mwandani wake wa siasa kwenye mji mkuu Harare, Mugabe alisema;
"Wacha turejeshe hukumu ya kifo, watu wanacheza na kifo kwa kuuana. Tunataka nchi iwe na amani na yenye furaha na sio nchi ambapo watu wanuana."
Zaidi ya wafungwa wamehukumiwa kifo, kwa mjibu wa ripoti za AP.
@habari na bbc swahil
No comments:
Post a Comment