ARUSHA.
Wakuu
wa mikoa ya Arusha na Manyara wamewataka walimu wa shule za msingi na sekondari
katika mikoa hiyo kutopokea michango yoyote kutoka kwa wazazi, watakaobainika
watachukuliwa hatua kali.
Mrisho
Gambo wa Arusha na Alexander Mnyeti wa Manyara wamesema kukusanya
michango hiyo ni kwenda kinyume na mpango wa elimu bure.
Gambo
ametoa kauli hiyo katika kikao na wadau wa elimu wilaya ya Karatu, kubainisha
kuwa imeibuka tabia ya baadhi ya wakuu wa shule kushirikiana na bodi za shule
kubuni utitiri wa michango.
Kwa
upande Mnyeti akiwa katika ziara ya siku saba wilayani Simanjiro, amepiga
marufuku michango hiyo na kuacha maagizo kwa wananchi, walimu na viongozi
wa ngazi ya wilaya na vitongoji.
Amesema
ni marufuku walimu kuchangisha fedha na kama kamati za shule na bodi zikiona
kuna ulazima zitoe michango ofisi za kata.
Chanzo:
mwananchi
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment