NSIMBO.
WAKAZI wa kata ya Katumba Halamshauri
ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi wameilalamikia serikali kwa kutoshughulikia
tatizo la maji kata ya katumba ambapo kwa sasa hawana maji kwa muda wa miezi 6.
Wakazi hao wametoa malalamiko hayo kwa Nyakati tofauti wakati
wakizungumza na Mpanda Radio kuhusu tatizo la maji linalowasumbua kwa sasa
ambapo wamesema limesababishwa na mashine iliyokuwa ikisukuma maji kuharibika.
Mwenyekiti wa jumuia ya watumia maji
Bw.Ngeze Joel amekiri kuwepo kwa tatizo hilo akisema tatizo la maji limetokana
na kuharibika kwa mashine huku Afisa Mtendaji wa vijiji vya Mnyaki A na Mnyaki
B Kombo Masatu amesema baadhi ya vifaa vimenunuliwa ili kumaliza tatizo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Ndui
Stesheni Hussein Nasri mahali Mashine hiyo ilipo kwa upande wake amesema hakuna
mwelekeo wa lini ufumbuzi utapatikana.
Kwa mjibu wa Bw.Hussein Nasri Mashine
hiyo yenye thamani ya karibu shilingi milioni 80 inasamabaza maeneo ya huduma
za jamii kama soko,shule,kituo vya polisi na sehemu nyingene muhimu.
Source: Issack Gerald
No comments:
Post a Comment