BARAZA la madiwani
katika halmashauri ya wilaya ya Uvinza mkoa wa Kigoma limemuagiza Mkaguzi mkuu
wa hesabu za ndani wa wilaya hiyo kufuatilia upotevu wa pesa ndani ya
vituo 9 kati ya vituo 30 ambavyo vilipokea fedha taslimu mil.300
kutoka kwenye mpango wa BRN mwaka 2016 kwa ajili ya ukarabati wa majengo
na ununuzi vya huduma za afya wilaya ni humo.
Hatua hiyo imechukuliwa
baada ya Upotevu wa fedha kiasi cha mil.1.8katika
kituo cha afya cha Igalula kilichopo kata ya Igalula na mil.1.9 katika kituo cha afya Basanza baada ya mkaguzi John Nyakiha
kupitia hesabu za matumizi ya fedha hizo na kugundua upetevu huo.
Kwa upande wa madiwani
wa halmashauri ya Uvinza wa kiwakilishwa na diwani kata ya Nguruka Abdahla
Masanga ameeleza wasiwasi wao ni uwezo mdogo wakamati katika matumizi ya fedha
na idadi ndogo ya watumishi katika vituo vya afya na hivyo kusababisha upotevu
wa pesa hizo.
Nae Mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya Uvinza Jackson Mateso ametaka elimu itolewe kwa wanchi
kuhusu fedha hizo kwani ziko chini ya mikono yao huku serikali ikiendelea
kufanya uchunguzi juu ya upotevu wa fedha hizo .
Source:Isack Isack
No comments:
Post a Comment