Shirikisho
la vyama vya watu wenye ulemavu Mkoani Katavi (SHIVYAWATA)limesema mpaka sasa
hawana uhakika wa kufanya maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu Duniani kwa
sababu ya uhaba wa bajeti
Kauli
hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa shirikisho hilo Bw.Issack Mlela wakati
akizungumzia maandaliza ya maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu
inayaotarajiwa kuadhimishwa Desemba 3 mwaka huu.
Kwa
upande wake Katibu wa chama cha watu wenye ulemavu mkoani Katavi Bw.Godfrey
Sadara pamoja na kuitaka jamii kuwafichua watu wenye ulemavu waliofichwa
majumbani pia amesema unyanyapaa unaoendelea dhidi ya kundi hilo linatakiwa
kukemewa na kila mmoja.
Asasi
ya kiraia ya IFI inayohusika na masuala ya watu wenye ulemavu mkoani Katavi
kupitia kwa mratibu wake Raphael Fortunatus imesema bado serikali ni kama
imesahau makundi ya watu wenye ulemavu katika kuwawezesha ili wafanye
maadhimisho.
Kitaifa
maadhimisho haya yanatarajia kufanyika Mkoani Simiyu Disemba 3 mwaka huu na
Kauli mbiyu ni Badilika tunapoelekea jamii Jumuishi na imara kwa watu wote.
Source:Issack Gerald
No comments:
Post a Comment