Baadhi ya wananchi mkoani katavi wamesema ni vyema jamii kubadili
tabia ikiwemo kuachana na ngono zembe ili kuweza kuepukana na maambukizi ya
virusi vya ukimwi
Mapema leo hii Wakizungumza na Mpanda radio namna wanavyoielewa siku ya ukimwi duniani wananchi
hao akiwemo Mwajuma Idd Bakary na Islam Said wamesema elimu kuhusiana na
ugonjwa wa ukimwi wamekuwa wakiipata na wameweza kuwahamasisha wengine kupima
afya zao
Sanjari na hayo pia wamewaasa vijana kuhakikisha wanapima afya zao
mara kwa mara na kuwa mabalozi kwa wengine namna ya kujiepusha na maambukizi
mapya ya Ukimwi
Siku ya ukimwi duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 1 ya kila
mwaka na kauli mbiu kwa mwaka huu inasema
“Changia mfuko wa maisha, Tanzania bila
Ukimwi inawezekana”
SOURCE;Safina Joel
No comments:
Post a Comment