Mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa katavi kamanda Damasi Nyanda |
KATAVI.
Mkuu wa jeshi la polisi
mkoa wa katavi kamanda Damasi Nyanda amewataka wananchi kusherekea kwa amani Sikukuu zinazokaribia na kufuata sheria
zilizowekwa.
Ameyasema hayo wakati
akizungumza na Mpanda Redio na kueleza kuwa jeshi la polisi limejipanga vizuri ili
kuhakikisha wananchi wanasherehekea kwa amani bila kuwepo na uvunjifu wa amani.
Aidha amewataka wazazi
kuwa makini na watoto wao hasa katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu na
kutoa ovyo kuwa watoto hawaruhusiwi kuingia maeneo ya disco.
Wananchi wamekuwa
hawaripoti baadhi ya viashiria vya matukio ya uharifu ambayo baadaye yamekuwa
yakisababisha madhara suala ambalo amewataka pia kuripoti taarifa hizo.
Chanzo:Issack Gerald
Chanzo:Issack Gerald
No comments:
Post a Comment