KINSHASA
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR limesema limeshtushwa na mapigano yanayoendelea Mashariki mwa Demokrasia ya Congo, hivyo kusababisha wimbi kubwa la wakimbizi kutoka nchini humo wanaoingia katika nchi jirani kama vile Burundi, Tanzania na Uganda.
Maelfu ya watoto, wanawake na wanaume wameacha makazi yao huku mapigano dhidi ya makundi yenye silaha ya Mai Mai yakiendelea Kusini mwa Jimbo la Kivu.
Kwa mujibu wa Shirika la
UNHCR, mpaka sasa, wakimbizi wapatao 1200 wameingia nchini Tanzania.
Wakati huo huo, inaamika kwamba, kuna wimbi kubwa zaidi za wakimbizi ambao wapo Kivu Kusini wakiwa katika hali mbaya ya kukosa chakula na makazi.
Bi Joan amesema, wakimbizi hao
wamekuwa wakiingia nchini Tanzania kwa kutumia Ziwa Tanganyika, huku wakiwa
wamechoka na baadhi wakiwa katika hali mbaya ya kiafya.
Chanzo: Bbc swahili
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment