Taifa la Korea Kaskazini linatarajiwa kuandaa maadhimisho ya 70 ya gwaride la jeshi lake kabla ya kufanyika kwa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi nchini Korea Kusini.
Gwaride la kila mwaka la Pyongyang linaloadhimisha kuanzishwa kwa jeshi la Korea Kaskazini limekuwa likifanywa kila mwezi Aprili kwa kipindi cha miaka 40.
Hatahivyo vyombo vya habari nchini humo vilitangaza mapema mwaka huu kwamba tarehe ya kufanyika kwa gwaride hilo la kijeshi imebadilishwa hadi Februari 8.
Korea Kaskazini imepuuzilia mbali ukosoaji wa mpango wake ikisema kuwa hakuna mtu aliye na uwezo wa kuishutumu.
''Ni utamaduni na swala muhimu sana kwamba kila taifa duniani linasherehekea uzinduzi wa jeshi lake' , kilisema chama tawala cha wafanyikazi Rodong Sinmun.
Marekani imesema kuwa ingependelea gwaride hilo kutofanyika kwa kuwa kwa sasa watu wanalenga michezo ya Olimpiki.
Siku ya Alhamisi, Korea Kaskazini ilisema kuwa haina mpango wa kukutana na maafisa wa Marekani , kulingana na chombo cha habari nchini Korea Kaskazini KCNA.
Serikali ya Korea Kusini imesema kuwa mwezi uliopita kwamba wanajeshi 13,000 na vifaa 200 vilipatikana karibu na uwanja wa ndege wa Pyongyang katika kile kinachoonekana kuwa gwaride la majaribio.
Wataalam wanasema Korea Kaskazini inatarajiwa kuonyesha silaha zake za masafa marefu.
''Kile tunachotarajiwa kuona katika gwaride hilo la kijeshi ni magari ya kubeba silaha, idadi yake na iwapo yanabeba silaha mpya'' , alisema David Schmerler, mchanganuzi wa Korea Kaskazini katika kituo cha James Martin cha masomo ya kuzuia kusambaa kwa silaha.
Chanzo:Bbc swahili
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment